SIMANZI KUBWA KWA MZEE YUSSUF NA WANAWE …mazishi ya mkewe ni Jumapili hii saa 7 mchana


Mzee Yussuf yuko kwenye simanzi kubwa sana baada ya kufiwa na mkewe wa pili (Chiku) na kumwachia watoto wawili.

Mbali na kufiwa na mkewe, Mzee Yussuf pia amepoteza kichanga chake ambaye naye alifariki sambamba na Chiku.

Mke wa Mzee Yussuf alifariki katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam Jumamosi jioni kwa matatizo ya uzazi ambayo pia yalimpoteza mtoto wa kiume aliyezaliwa.

Msiba uko nyumbani kwa familia ya marehemu, Kariakoo mtaa wa Livingstone ambapo mazishi ya mama na mtoto yatafanyika leo Jumapili saa 7 mchana katika makaburi ya Kisutu.
Saluti5 ilikuwepo nyumbani hapo Jumamosi usiku na kumshuhudia Mzee Yussuf akiwa mnyonge sambamba na watoto wake wawili wa kike (kama wanavyoonekana pichani.

Watoto hao ndio ukumbusho na faraja aliyoachiwa Mzee Yussuf na mkewe Chiku.

Mzee Yussuf ameiambia Saluti5 kuwa alikuwa anatamani sana marehmu amzalie mtoto wa kiume na alipanga kumwita Yunus, lakini mipango ya Mungu imekwenda kinyume na utashi wake.

“Tumshukuru Allah, maana yeye ndiye mpangaji wa kila jambo,” alisema Alhaj Mzee Yussuf, mwimbaji nyota wa taarab aliyestaafu.
Alhaj Mzee Yussuf akiwa na binti zake aliozaa na marehemu Chiku

No comments