SIMBA KUMTANGAZA NIYONZIMA KWENYE SHEREHE ZA "SIMBA DAY"

UONGOZI wa klabu ya soka ya Simba umeahidi kutangaza rasmi usajili wa kiungo mshambuliaji Mrwanda, Haruna Niyonzima baada ya mchezaji huyo kumaliza mkataba wake wa kuchezea Yanga.

Niyonzima ambaye mkataba wake na Yanga unamalizika Julai, mwaka huu anajiunga kujiunga Simba kwa kitita cha dola 80,000 za Kimarekani, sawa na mil 179 na kukubali kusaini mkataba wa miaka miwili baada ya kushindwana na Yanga ambao wanadaiwa walitaka kumpa kiasi cha dola mil 60,000, sawa na sh. mil 134 za Kitanzania.

Niyonzima ambaye ni kipenzi cha wana Yanga inadaiwa anatarajiwa kutambulishwa rasmi na timu yake mpya katika sherehe za Simba Day Agosti, mwaka huu.

Akiongea na saluti5, mwenyekiti wa kamati ya usajili, Zacharia Hans Poppe alisema klabu hiyo haitavunja sheria na utaratibu wa kutangaza usajili wa mchezaji huyo ambae bado ana mkataba na klabu yake.

“Wachezaji wengi bado wana mikataba, mnataka tuwatangaze usajili wao ili tuingie kwenye matatizo, tusubiri tu muda ukifika tutamtangaza huyo mnaemtaka.”

“Mashabiki wafikirie wanachotaka kufikiria ila Simba hatuwezi kumtangaza mchezaji ambaye yuko kwenye mkataba,” alisema Poppe.

Baada ya Simba kudaiwa kukamilisha usajili wa Niyonzima, kiungo huyo atapewa jezi namba 8 ambayo ilikuwa ikivaliwa ikivaliwa na Mwinyi Kazimoto.

Haruna kwa hivi sasa yuko mapumzikoni kwao nchini Yanga ambako amefunga mdomo kwa kutozungumza na chombo chochote cha habari ingawa tetesi ni kwamba atajiunga na wekundu wa Msimbazi.


Hivi karibuni aliliambia gazeti la Rwanda Time wakati akiwa na timu ya taifa kuwa, anaangalia kwenda kwenye changamoto mpya baada ya kukaa Yanga kwa miaka sita.

No comments