SIMBA SC KUJA NA VIKOSI VIWILI BALAA MSIMU UJAO

FUNGA kazi! Hii ndio kauli ya Kamati ya Usajili ya klabu ya soka ya Simba, ambapo imepanga kufanya usajili wa wanandinga wenye kiwango na uwezo unaofanana katika kila namba ili kupatikana kwa vikosi viwili hatari.

Hii inatokana na mkakati wa makocha Joseph Omog na msaidizio wake Jackson mayanja ambao ripoti yao ndio inayofanyiwa kazi na kamati hiyo ya usajili chini ya kamanda Zacharia Hans Poppe.

Wawili hwa wametangaza vita ambayo haina masihara hata kidogo katika usajili unaoendelea hivi sasa kwani wana hasira ya mambo yaliyojitokeza msimu uliomalizika hivi karibuni.

Makamu wa rais wa klabu ya Simba, Geoffrey Nyange “Kaburu” ameiambia saluti5 namna uongozi unavyoifanyia kazi ripoti ya makocha juu ya usajili wa msimu huu.

Akizungumzia suala hilo, Kaburu alisema dhamira ya timu ya Simba ya kupata vikosi viwili ndio inayotumika kama dira ya usajili unaoendelea hivi sasa na hakuna kulala hadi litimie hilo linalokaribia kutimia.

“Kazi ya usajili ndio kwanza inaanza ya kusuka kikosi kabla ya kuanza kwa Ligi msimu ujao, tunataka kila namba iwe na wachezaji wawiliwawili,” alisema Kaburu.


Aliongeza kuwa, kazi hiyo inatarajiwa kumalizika kabla ya kufanyika kwa sherehe maalum ya siku ya Sim,ba “Simba Day” ambayo hufanyika kila ifikapo Agosti 8, ambayo huwa mahususi kwa ajili ya kutambulisha “majembe” mapya ya msimu.

No comments