SIMBA SC WAISAKA SAINI YA KIUNGO WA AFC LEOPARDS

KIWANGO cha kiungo AFC Leopards, Allan Katelegga kwenye michuano ya Super Cup imewavuta Simba na sasa wanataka kunasa saini ya nyota huyo wa Kenya.

Kiungo huyo aliingia kipindi cha pili katika mchezo wa Super Cup dhidi ya Singida United na kutoa pasi ya bao kwa Vincent Obulu aliyeisababishia ushtimu yake na kutinga nusu fainali kwa mikwaju ya matuta 5-4 akiwemo kwenye orodha ya wapigaji.

Katika mchezo wa nusu fainali aliisumbua sana safu ya ulinzi wa Yanga ingawa mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 0-0 na Leopards kutinga fainali kwa kushinda mikwaju ya penati 4-2 ambayo pia katelegga alipiga na kumtesa mlinda mlango Deogratius Munishi “Dida”.

Pamoja na Simba kunyemelea saini ya mchezaji huyo, nao Singida united wanataka kuendelea kujenga kikosi chao kwa kumnasa mchezaji huyo.

Akizungumza jana, Kateregga aliosema tayari ameanza kufanya mazungumzo na viongozi wa Simba na Singida United walitaka asajili kwenye klabu kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara.

“Nimefanya mazungumzo na viongozi wa Simba na Singida United, lakini viongozi wa Simba ndio naona kama wanahitaji zaidi kunisajili, kwa hiyo nawasubiri tuweze kukubaliana na kucheza Tanzania,” alisema Katelegga.


Katelegga aliongeza kuwa mkataba wake na AFC Leopards umebakiza miezi sita kumalizika hivyo kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), zinamruhusu kufanya mazungumzo na klabu yoyote inayohitaji kumsajili.

No comments