SIMBA SC YAJIPANGA KUMFUNGA PINGU JUUKO MURSHID

BAADA ya beki wa kati wa Simba Mganda Juuko Murshid kupata timu nje ya nchi, uongozi wa wekundu hao umepanga kumuongezea dau mchezaji huyo ili aendelee kukipiga kwenye klabu hiyo.

Kabla ya kumalizika kwa mzunguuko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, kulikuwa na tetesi kwamba beki huyo anatarajia kuondoka Simba baada ya kupata timu Ulaya.

Hata hivyo taarifa zinasema kuwa sio rahisi kwa mchezaji huyo kuondoka Simba na uongozi umekuwa ukimjadili kila mara kuona uwezekano wa kumuongezea dau litakalozidi hiyo klabu inayomwitaji.

Chanzo hicho kilisema sio kama Juuko hapendi kubaki Simba, wanachopishana na uongozi ni kuhusu mshahara kwakuwa analipwa kiwango cha chini kuliko hata Mwanjani ambaye muda mwingi alikuwa benchi.

Alisema, kinachowafanya Simba wahahe kumbakiza mchezaji huyo ni kutokana na michuano ya kimataifa wanayotarajia kushiriki ambapo imeonekana ni beki atakayeisaidia timu hiyo kulingana na uzoefu wake.


”Mikakati iliyopo sio rahisi Juuko kuondoka Simba kwa kuwa anaonekana ni beki mwenye mzoefu wa michuano ya kimataifa kuliko kusajili mwingine, hivyo ishu inayoendelea ni kuona jinsi gani ya kumuongezea mshahara ikizingatiwa Simba sasa hivi pesa ipo ya kumbakisha,” kilisema chanzo hicho.

No comments