SIMBA WAPANIA KUIKOSESHA USINGIZI YANGA

SIMBA inaimarisha kikosi chake katika kuhakikisha msimu ujao inakuwa katika ubora wa hali ya juu.

Na katika kusaka wachezaji wapya ambao mashabiki wao wameamua kuubatiza jina la “sakasaka” Simba imeamua kwa mara ya kwanza kuwakosesha usingizi mashabiki wa Yanga.

Simba tayari wameshajibu mashambulizi ya Yanga ambao walitangulia kumsajili Ibrahim Ajib na wao wakahakikisha kwamba wanaibomoa Yanga.

Kombora la kwanza kutua Jangwani ni kumsajili Haruna Niyonzima ambaye wiki iliyopita, Yanga walisalimu amri kwamba wameshindwa kuendelea naye baada ya kiungo huyo raia wa Rwanda kuidai Yanga mpunga wa maana zaidi ambao hawana.

Habari zinasema kwamba Simba wameshamalizana na kiungo huyo fundi na baada ya mkataba wake wa kuitumikia Yanga kumalizika Julai 21, mwaka huu hatatambulishwa rasmi.

Lakini wakati kovu la Niyonzima lingali bichi, Yanga hawana amani baada ya kusikia kwamba Simba wamefanya mazungumzo na wamefikia mahali pazuri mshambuliaji Donald Ngoma raia wa Zimbabwe.

Ngoma ambaye mkataba wake wa kuichezea Yanga umemalizika, madaiwa kuwa katika hatua ya mwisho ya kutua Simba, na kwamba wakati wowote kuanzia sasa atasaini mkataba.

Tishio hilo linawatisha Yanga, lakini wanachokiogopa zaidi ni habari kwamba licha ya Ngoma, Simba wana mpango wa kumsajili nyota wa Yanga jina lake linafanywa siri.

Habari hizi zinawaweka Yanga katika joto kubwa, na wamekuwa na wasiwasi kwamba huenda jina linalofichwa likawaumiza zaidi Yanga.

Hata hivyo wapenzi wenyewe wa Yanga wamekuwa wakihusisha hatua ya kiungo ya mshambuliaji Simon Msuva ambaye anaomba kuuzwa nje ya nchi kamba ndiye anayewindwa na Simba.

Wanachosema Yanga ni Msuva akiruhusiwa kuondoka tu Yanga maana kuwa huru na Simba wanakwenda kumchukua hukohuko Morocco anakodaiwa kwenda.

Msuva anadaiwa kuwindwa na klabu ya Waydat Casablanca ya Morocco ambako ameahidiwa mshahara unaofikia shilingi milioni 9 za Kitanzania.


Wasiwasi huo umekuwa ukiwanyima usingizi Yanga ambao katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakuomba viongozi wao wasimuuze nyota huyo maanayake watakuwa wamehruhusu Simba kumchukua.

No comments