SIMBA YAMTUMIA TIKETI OKWI KUTUA BONGO DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya Simba umeeleza kuwa tayari umeshamtumia tiketi mshambuliaji wake, Immanuel Okwi raia wa Uganda ili kujiunga na kikosi hicho tayari kwa kumalizia mzunguuko wa kwanza.

Awali Simba iliripotiwa kutaka kumrejesha Okwi Msimbazi kwa msimu ujao baada ya kumalizana na klabu yake ya SC Villa iliyokuwa na mkataba nae wa miezi sita.

Kwa sasa Okwi yuko kwenye kikosi cha timu yake ya Uganda iliyocheza juzi na Cape Verde, katika michuano ya kuwania tiketi ya kushiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019, baada ya kuonyesha kiwango kikubwa cha soka.

Akiongea na saluti5, bosi mmoja wa Simba alisema uongozi wa klabu hiyo umeshamtumia tiketi Okwi na wakati wowote atatua nchini kwa ajili ya kumalizana na kabisa na Simba.

“Tunatarajia kumalizana nae mapema, hivyo tumeona tumtumie kabisa tiketi ili atakavyorejea Uganda na timu ya taifa aje moja kwa moja Dar es Salaam,” alidokeza bosi huyo.

Simba imekuwa ikisumbuka kutokana na nafasi ya mshambuliaji kutokuwa na mtu makini wa kutupia mabao na kila mmoja anaamini kuwa Okwi atakuwa mtu sahihi kwenye nafasi hiyo.


Taarifa zimekuwa zikisema kuwa endapo Okwi anayetarajia kutua nchini wiki hii, atakuja basi kuna uwezekano mkubwa mshambuliaji Fredrick Blagnon akafunguliwa mlango wa kwaheri.

No comments