SINGIDA UNITED YASEMA HAINA MPANGO WA KUWASAJILI IBRAHIM AJIBU WALA DEUS KASEKE

KLABU ya Singida United ambayo inaendelea na maandalizi ya Ligi Kuu msimu ujao, imesisitiza kuwa kwa sasa haifikirii kusajili wachezaji wanaotamba kwenye klabu kubwa.

Mkurugenzi wa Singida United, Festal Sanga amesema kuwa, licha ya baadhi ya wachezaji kutoka timu kubwa kuhusishwa kujiunga na timu yake, lakini bado kwa upande wao hawana mpango huo.

“Kikubwa kwanza mashabiki na wadau wa soka watarajie mabadiliko makubwa ya klabu yetu ambayo imepanda daraja, kwamba italeta changamoto kubwa kwenye msimu ujao,” alisema Sanga.

“Kingine ni kwamba katika kipindi hiki cha pre season pia watu wategemee kwamba tutafanya usajili mbalimbali wa wachezaji, wengine ni wachezaji ambao watu hawategemei kama wanaweza kutua Singida United, kwahiyo kuna mambo makubwa yanakuja.”

“Sisi hatujasajili wachezaji wengi sana, kwenye orodha yetu ya mwongozo wa usajili tunatarajia kusajili wachezaji saba wa kimataifa na saba wa ndani ambao watakuja kuungana na wale 11  walioipandisha timu kutimia 25 tunaowahitaji.”


“Hizi tetesi zinazoendelea kwamba kuna wachezaji kama Ibrahim Ajib, Dues Kaseke ni tetesi tu lakini kimsingi sisi kama klabu hatulengi sana katika kuwaangalia wao,” alisema Sanga.

No comments