SNURA ASEMA SHEPU YAKE NI YA ASILI SIO "MCHINA"... adai familia yao wote "mashaallah"

STAA wa muziki wa kizazi kipya, Snura Mushi amesema kuwa hajawahi kutumia dawa za kuongeza shepu kama inavyoelezw na watu kwenye mitandao ya kijamii.

Snura alisema kuwa hayo ni maumbile yake ya asili kwani hata familia yao wote wana maumbile makubwa.

“Jamani huu ni mwili wangu, hata ukifika kwetu utaona namna ambavyo tumejaaliwa kuwa na maumbile makubwa. Sijatumia dawa yoyote,” alisema Snura.

“Wanaosema nimetumia mchina ni kwa sababu hawaufahamu ukoo wangu, kwetu sisi wote tuna miili mikubwa.”


Msanii huyo aliongeza kuwa anafahamu ni kinyume cha maadili ya Mungu kubadilisha maumbile ya asaili, hivyo kamwe hawezi kufanya dhambi hizo.

No comments