SSERUNKUMA APATA DILI NCHINI MOROCCO... ni katika klabu ya Ittihad Riadi Tanger ya Ligi Kuu

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Mganda Dan Sserunkuma amepata dili la maana nchini Morocco baada ya kusajiliwa na klabu ya Ittihad Riadi Tanger inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter Sserunkuma alithibitisha kuingia mkataba na klabu hiyo ambapo aliwashukuru wachezaji wenzake wa Bandari FC nchini Kenya aliyokuwa akiichezea pamoja na familia yake.

Sserunkuma alisajiliwa na Simba kipindi cha usajili wa dirisha dogo la msimu wa 2014/15 akitokea Gor Mahia ya nchini Kenya lakini alijikuta akifungashiwa virago kutokana na kutoridhi matarajio ya wekundu hao.

Katika mtandao wake huo wa Twitter, sserunkuma ambaye ni raia wa Uganda aliandika: “Ni rasmi sasa kwamba mimi ni mchezaji wa Ittihadi Riad Tanger. Namshukuru sana Mungu kwa hilo, naishukuru familia yangu, wakala wangu na mashabiki wangu wote, nawashukuru pia wachezaji wenzangu wa Bandari FC kwa upendo wao kwangu.”


Sserunkuma aliifungia Simba mabao mawili pekee kwenye Ligi Kuu bara kabla ya kutimliwa.

No comments