STEVEN GERRARD AWEKA BAYANA AZMA YAKE YA KUFUNDISHA LIVERPOOL

HIZI ndizo ndoto alizonazo Steven Gerrard ambaye ameweka bayana kuwa iko siku atarejea Anfield lakini sio kusakata kabumbu bali kama kocha.

Akinukuliwa na Sky Sports, Gerrard alisema alipokuwa bado mchezaji kijana wa Liverpool amewahi kuweka bayana azma ya kutaka kusomea ukocha na sasa anadhani muda wa kutimiza malengo hayo unakaribia.

Alisema, hatua ya kuwa mchezaji maarufu na mwenye jina kubwa imeshapita, lakini kilichobaki ni kutimia kwa ndoto ya kuwa kocha mwenye mafanikio ulimwenguni.

“Wakati ule nilikuwa natimiza majukumu ya kuwa nahodha na mchezaji, lakini sasa ninapambana kwa ajili ya kuwa meneja.”

“Nani anajua kama nitaweza kuwa meneja wa Liverpoo, ni ndoto yangu kubwa lakini ni suala la kuwa bora kwa sasa na baadae.”

“Sio suala la kusema unataka umeneja ama unataka kuwa meneja, bali ni kwa kupitia safari ndefu hadi mafanikio.”
“Kama unataka umeneja lazima ujitoe na kuthibitisha kwa uwezo wako binafsi.”

“Ni safari ndefu baadae, bado nina miaka michache kuacha kucheza na huo ndio mtazamo wangu kwa sasa.”


“Walio makocha leo wamepitia mitihani na safari ndefu kabla ya kufikia malengo, mafanikio na ndoto kama yangu. Nami ninapita katika hatua zote muhimu,” alisisitiza Gerrard.

No comments