STRAIKA WA MALAWI ANAYETAMANIWA NA KLABU NYINGI ACHAGUA KUTUA MSIMBAZI

STRAIKA raia wa Malawi, Boniface Kaulesi yuko katika kuwindwa na timu mbalimbali za ndani na nje ya nchi yake, lakini mwenyewe anataka kukipiga katika kikosi cha wekundu wa Msimbazi, Simba.

Awali taarifa kuhusu kiungo huyo zilisema alikuwa anatakiwa na Yanga na alitajwa katika orodha ya usajili huo unaoendelea.

Taarifa za kutoka nchini Malawi zinasema kuwa Kaulesi anayekipiga katika klabu ya Red Lions amewaeleza marafiki zake wa karibu kuwa ana ndoto ya kuja kusakata soka nchini Tanzania, lakini ni ndani ya kikosi cha “Mnyama”.

Wakala wa wachezaji nchini Malawi, Zacharia Huns ameweka bayana azma ya kiungo huyo kutaka kuichezea Simba na kwamba ndoto yake hiyo ameiweka bayana hata kwa watu wake wa karibu.

Kiungo huyo amekuwa akitajwa kama kati ya viungo mahiri zaidi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya nchini Malawi ambaye ni tegemeo.


“Huyu anatakiwa na Simba ambayo ni kati ya timu kubwa za Tanzania, anaweza kwenda kwenye timu hiyo,” alisema wakala huyo.

No comments