TIEMOUE BAKAYOKO USAJILI WA KWANZA CHELSEA


CHELSEA inakaribia kushinda mbio za kuwania saini ya kiungo wa ulinzi wa Monaco, Tiemoue Bakayoko.

Gazeti la Daily Mail limedai kwamba uhamisho wa kiungo huyo utaigharimu klabu hiyo bingwa wa Premier League pauni milioni 35 baada ya Antonio Conte kuweka wazi kuwa anamtaka Stamford Bridge staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa.

Chelsea tayari imeshakubaliana na Monaco juu ya ada ya kiungo huyo ambaye atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na mabingwa hao wa England katika dirisha hili la kiangazi.

Bakayoko pia alikuwa akitakiwa na Manchester United na Arsenal, lakini ripoti kutoka Ufaransa zimedai kuwa kiungo huyo wa miaka 22 ameonyesha nia ya kutaka kufanya kazi chini ya Conte.

No comments