KLABU ya Torino ya Italia inapigana vikumbo na baadhi ya klabu zinazomfukuzia mlinzi wa Villareal, Adrian Gomez ambaye kwa sasa anakipiga kwa mkopo katika timu ya CD Leganes inayoshiriki La Liga nchini Hispania.

Gomez amekuwa akihusishwa na kujiunga na PSG katika usajili ujao wa dirisha la kiangazi.

Lakini Torino itawalazimu kuweka dau la ziada mezani la pauni mil 24 kwa ajili ya jembe hilo.

Klabu hiyo inawabidi kupambana kwa ajili ya beki huyo kisiki kwani anawaniwa kwa karibu pia na timu za Monaco na AC Milan.

Lakini taarifa zinasema kuwa Torino wameshamaliza mazungumzo ya awali na Gomez kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao kinachopambana kwa ajili ya ubingwa wa msimu huu.


Awali,Monaco waliweka mezani dau la pauni mil 15 kwa ajili ya mlinzi huyo kabla ya Villareal hawajaweka bayana kuwa dau la mchezaji huyo ni mil 23.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac