TWANGA PEPETA, MASHAUZI CLASSIC JUKWAA MOJA IDD MOSI MANGO GARDEN … ‘bifu’ lao kuibuka tena?


Bendi ya The African Stars “Twanga Pepeta” pamoja na Mashauzi Classic, zitaumana jukwaa moja siku ya Idd Mosi ndani ya Mango Garden, Kinondoni.

Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka na mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Mashauzi wote kwa nyakati tofauti wameithibitishia Saluti5 kuwa bendi zao zitaonyeshana kazi Mango Garden siku ya Idd Mosi.

Mara ya mwisho bendi hizo mbili kuumana Mango Garden ilikuwa ni Machi 28 mwaka jana ambapo upinzani mkubwa uliibuka na kupelekea bifu la chini chini baada ya onyesho hilo.

Licha ya kuwa bendi hizo mbili zinapiga aina tofauti ya muziki, lakini zinapokutana jukwaa moja huwa ni patashika si la kitoto.

Je bifu hilo litarejea tena Idd Mosi? Wakurungezi wa bendi hizo mbili zinazoutumia Mango Garden kama ukumbi wa nyumbani, wamesema nyingi wao ni ndugu moja ingawa upinzani hautakosekana.

No comments