"TYSON FURY SASA YUKO FITI KUREJEA ULINGONI"

MJOMBA wa binga wa uzito wa juu duniani raia wa England, Tyson Fury, aitwaye Peter, amesema mara baada ya kuwa nje ya ulingo kwa muda mrefu kutokana na msongo wa mawazo, hatimaye mwanaye huyo yupo fiti kurejea ulingoni kurudisha heshima yake.

Peter amesema kuwa mara baada ya kupita katika kipindi kigumu katika maisha, mwanaye huyo ameamua kuachana na ulevi pamoja na matumizi ya dawa za kulevya ambazo ndizo zilikuwa chanzo cha bondia huyo kupotea.

Mbali na mkali huyo, lakini Peter ni mwalimu wa binamu yake na Tyson, Hughie, ambaye pia ni bingwa wa uzito wa juu ambaye anakuja hivi sasa.

“Alikuwa katika kipindi cha mapunziko pamoja na familia yake lakini pia tayari amerejea katika ubora wake, natarajia kukaa naye chini na kumwekea ratiba mpya ambayo itamsaidia na kumjenga."


“Ninaamini hawezi kupotea tena mara baada ya kupewa ushauri na natarajia kumtafutia pambano kabla ya mwisho wa mwaka huu ili kumpima kama yale niliyokuwa namfundisha ameyashika na kuyafanyia kaza sana,” alisema.

No comments