UAMUZI WA ANTONIO CONTE JUU YA DIEGO COSTA WAWACHEFUA MASHABIKI WA CHELSEA

UAMUZI wa kocha wa mabingwa wa soka wa England, Chelsea, Antonio Conte kutamka kwamba anamtema rasmi mshambuliaji wa kikosi hicho, Diego Costa, umewaumiza mashabiki wengi wa kikosi hicho.

Kocha huyo wiki iliyopita alimtumia ujumbe mshambuliaji huyo akimwambia kwamba hayuko kwenye mipango yake msimu ujao, ujumbe ambao sio tu kwamba umemshitua Costa mwenyewe, lakini pia hata mashabiki wa Chelsea.

Gazeti la Daily Mail limeandika kwamba mashabiki wengi wa klabu hiyo nchini Uingereza wamekasirishwa na kitendo cha Conte kumtema Costa na wengi wao wanaamini kwamba kocha huyo ameteleza.

Mashabiki hao wamesema kwamba uamuzi huo unaivuruga klabu kwasababu nafasi ya Diego Costa katika kikosi hicho ni muhimu.

Kocha huyo alimtumia ujumbe mshambuliaji huyo akiwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania na
yeye mwenyewe amesema kwamba hashangazwi na uamuzi huo.

Costa amesema kwamba amefahamishwa na meneja wa klabu hiyo, Antonio Conte kwamba hayupo tena katika mipango ya klabu hiyo.


Costa, 28, alifunga mabao 20 katika mechi 35alizocheza Ligi Kuu Uingereza na kuisaidia Chelsea kushinda taji la Ligi hiyo, lakini sasa anaonekana kukaribia kuondoka Stanford Bridge.

No comments