UPANGAJI MAKUNDI NDONDO CUP 2017 WAMALIZIKA

ZOEZI la upangaji wa makundi ya Ndondo Cup 2017 limemalizika vizuri, huku mwaka huu kukiwa na mapinduzi makubwa kuanzia mapema kabisa ambapo hatua ya upangaji wa makundi na hafla nzima ya uzinduzi wa hatua hiyo ilionekana mubashara kupitia kituo cha Azam Tv katika Channel yao ya Azam Sport HD.

Kwa mujibu wa mratibu wa mashindano hayo, Shafii Dauda, kila kitu kilikwenda kama kilivyopangwa na kila mtu alishuhudia upangwaji wa makundi na kuridhika kwamba hakuna upendeleo wala magumashi katika draw hiyo.

Katika makundi hayo ilishuhudiwa makundi manane yenye timu nne kwa kila kundi na kufanya jumla ya timu zote kuwa 32.

Hata hivyo, kundi H ndio linatajwa kuwa kundi la kifo kutokana na kila timu mbili zilizopangwa kwenye kundi hilo kuwa na uhasama mkubwa kwenye soka.

Kundi la H linazikutanisha timu za Kauzu FC (Tandika), Faru Jeuri (Buguruni), Sheraton (Tandika) na Miami (Vingunguti).


Mechi ya ufunguzi inatarajiwa kupigwa Juni 17 kwenye uwanja wa Kinesi.

No comments