USAJILI WA VIRGIL VAN DIJK LIVERPOOL KUWEKA REKODI MPYA YA DUNIA


Liverpool inakaribia kuvunja rekodi mpya ya dunia ya usajili wa beki wa bei mbya, baada ya kutajwa kuwa ipo sehemu nzuri ya kumnasa beki wa Southapton Virgil van Dijk.

Sentahafu huyo wa kimataifa wa Holland anawaniwa pia na Manchester City na Chelsea, lakini inaaminika anataka kwenda Liverpool ambapo pauni milioni 60 zinatarajiwa kuwekwa mezani na miamba hiyo ya Anfield.

Kama usajili huo utafanyika, basi Liverpool watavunja rekodi ya pauni milioni 50 iliyowekwa na Manchester City miezi 12 iliyopita pale walipomnunua John Stones kutoka Everton.No comments