Habari

VICTOR LINDELOF AONGEZA IDADI YA WATAALAM WA ‘FREE-KICK’ MANCHESTER UNITED

on

Victor Lindelof amesajiliwa na Jose Mourinho ili kuimarisha safu ya ulinzi Manchester United msimu ujao, lakini sentahafu huyo wa kimataifa wa Sweden ana kitu cha ziada.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22, anatajwa kuwa ni fundi wa mipira iliyokufa (free-kick) na hivyo anategemewa kuongeza ushindani kwa  Paul Pogba, Juan Mata na Marcus Rashford katika eneo hilo.
Lindelof  aliyesajiliwa kwa pauni milioni 30.7, ameiambia MUTV kuwa yuko vizuri katika upigaji wa free-kick na hatamwangusha kocha iwapo atapewa jukumu hilo.

Moja ya mabao aliyofunga Lindelof kwa free-kick, ni lile lililoipatia timu yake ya Benfica bao la kusawazisha dhidi ya Sporting Lisbon msimu uliopita katika mchezo ulioisha kwa sare ya 1-1.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *