VICTOR WANYAMA APONGEZA BONGO KUWA NA VIPAJI VINGI VYA SOKA

KIUNGO wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya nchini England, Victor Wanyama ambaye kwa sasa yuko hapa nchini kwa mapumziko mafupi, amesema kuwa anapongeza uwepo wa idadi kubwa ya nyota wenye vipaji katika taifa hili.

Wanyama ambaye ni raia wa Kenya alizitaja baadhi ya timu anazozifahamu hapa nchini zikiwemo Yanga, Simba na Azam lakini pia anawafahamu nyota wengi wa hapa akiwemo Mbwana Samatta anayecheza soka la kulipwa Ubelgiji.

“Tanzania kuna vipaji vingi, hilo halina ubishi. Kwa sababu nyota wengi hapa nawafahamu na hata klabu kubwa nazijua, naamini iko siku inaweza kupiga hatua kubwa kisoka,” alisema Wanyama.

“Hii si mara yangu ya kwanza kuja hapa, nafahamu mazingira ya hapa, najua kila kinachoendelea katika soka la Tanzania,” aliongeza nyota huyo.


Victor Wanyama kabla ya kutua Tottenham aliwahi kuichezea timu ya Celtic ya Scotland na kuwa mchezaji wa kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kuibuka na goli kwenye mchezo dhidi ya Barcelona.

No comments