VICTORIA SOUND BAND NDANI YA ROSH GARDEN MWANDEGE EID EL FITR

VICRORIA Sound ‘Wana Chukuchuku Style’ wao wamepanga kusherehekea Sikukukuu ya Eid Fitr ndani ya Rosh Garden, Mwandege katika siku za Idd Mosi na Idd Pili, imefahamika.

Akiongea na saluti5, Kiongozi mwandamizi wa Victoria Sound, Jonas Mnembuka amesema kuwa wameamua kuangukia Mwandege katika shamrashamra za Eid el Fitr ili kutii maombi ya muda mrefu ya mashabiki wao wa huko.

“Tumepokea maombi mengi na ya muda mrefu ya mashabiki wetu wa Mwandege, Pwani ambao wameomba tuwapelekee burudani katika sikukuu ya Eid el Fitr, nasi hatuna budi kufanya hivyo,” amesema Mnembuka.


Kiongozi huyo amesema kuwa wameawaandalia mashabiki wao wa huko mambo mengi matamu ambayo anaamini yatawasuuza nafsi zao na kuwaacha wakiwa wamekongwa nyoyo kutokana na burudani watakayoitoa kuwa pevu zaidi.

No comments