VICTORIA SOUND WAREJEA SCORPION, MASEBUKA MBAGALA

BAADA ya kufanya makubwa kwenye shoo zake za Eid el Fitr ndani ya Rosh Garden, Mwandege, Pwani, bendi ya Victoria Sound ‘Wana Chukuchuku Style’ imetangaza kuendelea na shoo zake za kawaida kuanzia kesho Ijumaa.

Kiongozi wa Victoria Sound, Jonas Mnembuka amesema kuwa, bendi yake itatumbuiza kwenye ukumbi wa Scorpion Night Pub, Mbagala Charambe na keshokutwa Jumamosi watakuwa ndani ya Masebuka Bar, Mbagala Kizuiani.

“Tumerejea kwenye ratiba zetu za kawaida hivi sasa baada ya kumalizika kwa mfungo mtukufu wa Ramadhani na tunaomba mashabiki kutusapoti kwa kujitokeza kwa wingi kila tutakapotumbuiza,” amesema Jonas.

Jonas amesema kuwa kikosi chake kimejipanga kikamilifu kuhakikisha kinamwaga burudani ya kukata na shoka kwa mashabiki watakaohudhuria shoo zao hizo na kwamba watapokea maombi mbalimbali ya nyimbo na kuyafanyia kazi.


Amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kwani mbali na nyimbo za kukopi, pia watatambulisha vibao vyao vipya ambavyo ni maandalizi ya albamu yao ijayo anayoisifu kwa kusema itakuwa moto wa kuoteambali.

No comments