VIDEO YA MDUARA WA "MOYO KAMA MACHO" YA KIVURAND YAJA

KICHUPA cha wimbo wa mduara wa ‘Moyo kama Macho’ ulioimbwa na mfalme wa Kibao Kata, Jumaa Kivurande ‘Kivurande Junior’ iko njiani, imebainika.

Kivurande mwenyewe ameinyetishia saluti5 kuwa, video hiyo itafanywa na moja ya kampuni zenye uwezo mkubwa hivyo anaamini itakuwa na ubora wa hali ya juu na ambayo itakuwa mfano wa kuigwa.

“Nawaomba mashabiki na wapenzi wakae mkao wa kuisubiri kwa hamu video ya mduara wangu wa wimbo ‘Moyo Kama Macho’ ambayo natarajia kuifanya muda si mrefu,” amesema Kivurande.


Kibao hicho ambacho kimebeba ujumbe mzito wa kimapenzi juu ya namna moyo usivyochagua pahali pa kutua, kwa sasa ni kati ya nyimbo zinazosumbua kwenye radio mbalimbali pamoja na mitandao ya kijamii.

No comments