Habari

WAKALA WA JOSE MOURINHO AKUTANA NA FABINHO

on

WAKALA wa Jose
Mourinho, Jorge Mendes, ameonekana akipata chakula cha jioni na mteja wake
Fabinho Tavares (pichani), anayetajwa kufukuziwa na Manchester United, lakini mazungumzo
yao yaliegemea uhamisho wa nyota huyo kwenda Atletico Madrid.
Fabinho anayemudu
nafasi ya beki na kiungo ni mmoja wa wachezaji wanne waliobaki katika orodha ya
wanaofukuziwa na Mourinho baada ya kocha huyo kukamilisha usajili wa beki wa
kati wa Benfica, Victor Lindelof. Wengine ni straika wa Real Madrid, Alvaro
Morata, winga wa Inter Milan, Ivan Perisic na straika wa Torino, Andrea
Belotti.
Kwa mujibu wa
gazeti la AS, Mendes na Fabinho walikutana na Mtendaji Mkuu wa Atletico Madrid,
Miguel Angel Gil Martin katika hoteli moja maarufu katikati ya jiji la Madrid
Jumanne usiku, hivyo kuibua tetesi mpya kuwa anaweza kumkacha Mourinho na
kwenda kufanya kazi na Diego Simeone.

Kama nyota huyo
atachagua kwenda Atletico, atalazimika kusubiri hadi Januari mwakani aweze
kucheza kutokana na klabu hiyo kutumikia adhabu ya Fifa ya kutosajili wachezaji
wapya hadi mwakani baada ya kusajili wachezaji chini ya miaka 18.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *