WAKALA WA MORATA ASEMA WANAISIKILIZIA REAL MADRID TU

WAKALA wa mchezaji Alvaro Morata amesema kwamba kwa sasa mteja wake huyo wa klabu ya Manchester United wanaisikilizia Real Madrid ili itoe maamuzi kama itamuuza straika huyo.


Kwa sasa Man United inahusisishwa vikali kumnasa staa huyo wa timu ya taifa ya Hispania na taarifa zinaelweza kuwa wiki iliyopita ilituma ofa ya euro mil 60 ikakataliwa lakini kwa sasa kocha wa mashetani hao wekundu, Jose Mourinho ana mpango wa kutuma ofa mpya.

No comments