WAKALA WA YUSUPH NDIKUMANA ASEMA SIMBA INATUMIA "NJIA CHAFU" KUTAKA KUMSAJILI MCHEZAJI WAKE

SIMBA imesemekana kupata aibu kubwa ikifanya harakati za kumsajili beki wa Mbao FC, Yusuph Ndikumana baada ya wakala wa mchezaji huyo kutaja njia “chafu” zinazofanywa na mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa timu hiyo, Zacharia Hans Poppe.

Akiongea na saluti5, wakala wa Ndikumana, Dennis Kadito anayeishi Ufaransa alisema beki wake huyo alimfuata na kumwambia kwamba Simba wanamfuata Burundi kufanya nae mazungumzo ya kusaini mkataba ambapo mtu aliyefika nchini humo alikuwa ni Hans Poppe.

Kadito alisema mara baada ya Has poppe kufika Burundi aliwasiliana na Ndikumana ambaye alimtaka bosi huyo kuwasiliana na wakala wake katika kumaliza usajili huo lakini kigogo huyo hakutaka kufanya hivyo.

Aliongeza wakala huyo akisema aliamua kumpigia hans Poppe simu na kumuhoji kama amekwenda Burundi kumalizana na Ndikumana lakini kigogo huyo alikataa na kusema amekwenda katika biashara zake binafsi.

“Unajua Simba sijui wanachofanya nini, hawajui kwamba mimi nina mkataba na mchezaji na hataweza kusaini kokote bila ridhaa yangu. Sasa Hans Poppe yuko Burundi na anadai amekwenda kufanya mambo yake lakini Ndikumana amenipigia simu na kunambia anataka kumsajili.,” alisema Kadito.

“Hans Poppe hata kabla ya kuja Burundi alishampigia Ndikumana na kumwambia hayo yote kwamba anakwenda na mchezaji, akamwambia anatakiwa kuwasiliana na meneja wake. Wanamtaka mchezaji lakini hawataki kufuata utaratibu.”

No comments