WANACHAMA WA YANGA WASISITIZANA KUACHA KAULI ZA KUVURUGA UMOJA KLABUNI

WANACHAMA wa klabu ya Yanga wametakiwa kuacha malumbano yasiyokuwa na tija ambayo yanaweza kutibua hali ya amani ambayo imeanza kujitokeza baada ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya tatu mfululizo.

Baadhi ya wanachama wa Yanga ambao walikusanyika juzi makao makuu ya klabu hiyo Mtaa Twiga na Jangwani wameeleza hisia zao kuhusu kukerwa na wanachama wenzao ambao mara kwa mara wamekuwa wakizungumza na vyombo vya habari na kutoa kauli zinazoweza kuchochea mgawanyiko.

Ndani ya mabingwa hao wa Tanzania Bara kumekuwepo na makundi mawili yanayovutana, huku kundi moja huku kundi moja likihoji juu ya mkataba wa Sportpesa na lingine likionekana kuendelea kumuhitaji mwenyekiti aliyetangaza kujiuzulu, Yusuph Manji.

“Kuna baadhi ya watu hawana lengo zuri na klabu yetu, kila mara wanazungumza na vyombo vya habari wakitoa kauli zinazoweza kutugawa wanachama, huu si wakati wa kutoa kauli za namna hiyo,” alisema mwanachama Hashim Ally ambaye aliungwa mkono na wanachama wenzake. 

No comments