WASHAWASHA CLASSIC MIN BAND YASAMBARATIKA… wamiliki wake wagawana vyombo

TAARIFA rasmi zilizotufikia hivi karibuni ni kwamba bendi ya muziki wa mipasho iliyokuwa ikija juu kwa kasi ya Washawasha Classic Min Band imevunjika rasmi.

Mmoja wa waliokuwa viongozi wa bendi hiyo, Amour Maguru ameitonya saluti5 kuwa kiongozi mwandamizi mwenzake alimfuata ghafla na kumweleza kuwa wameona wavunje bendi kwa madai haoni faida yake.

“Nilijaribu sana kumdadisi kiongozi mwenzangu yule kuhusu uamuzi wake, lakini cha ajabu hakuwa na jibu zuri kwangu na badala yake alishikilia msimamo wake huo na kufanikiwa kuivunja bendi,” amesema Amour.


Amour amesema kuwa hivi sasa anajipanga upya kuona anaibuka na jambo gani jingine baada ya Washawasha kuingia ‘mdudu’ ambapo hata hivyo anawaomba radhi mashabiki ambao walishaanza kuikubali bendi hiyo.

No comments