WAZIR JUNIOR: MSIJALI, NITALETA KICHEKO AZAM FC

BAADA ya kuwa kwenye msimu wa hasara na ugumu kutokana na kukimbiwa na baadhi ya wachezaji wake muhimu ikiwa ni pamoja na kukosa kushiriki kwenye michuano ya kimataifa, hatimae mshambuliaji mpya wa Azam, Wazir Junior ametangaza kuifuta machozi timu hiyo ambayo ina uwekezaji mkubwa.

Azam ilifanikiwa kumnasa Junior na kumsanisha mkataba wa miaka miwili nyota huyo aliyetoka kwenye timu ya Toto African ya jijini Mwanza.

“Najua mipango ya klabu hii ni mikubwa ambayo inalenga kushiriki kwenye michuano ya kimataifa mwakani, hivyo ninaomba kupewa ushirikiano kutoka kwa wachezaji wenzangu pamoja na mashabiki ili kwa pamoja tuweze kusonga mbele,” alisema nyota huyo.

“Nadhani hapa ni sehemu nzuri kwangu, nitapigana kwa nguvu ili kuisaidia timu yangu kusonga mbele msimu ujao,” aliongeza.


Mshambuliaji huyo alifunga jumla ya mabao saba msimu uliopita akiwa na Toto African, alipewa jezi namba saba iliyokuwa inatumiwa na Kelvin Friday ambaye alikuwa kwenye timu ya Mtibwa Sugar ya mjini Morogoro kwa mkopo.

No comments