WENGER AHAHA KUMSHAWISHI OZIL KUSALIA EMIRATES... ataka kumpa kandarasi ya kuanzia miaka mitano

BAADA ya kukubaliwa kuongeza kandarasi ya miaka miwili ndani ya klabu ya Arsenal, kocha Arsene Wenger sasa yumo katika harakati ya kuwabakiza baadhi ya nyota wake muhimu akiwemo Mesut Ozil.

Sio kumbakiza tu nyota huyo bali Wenger yuko katika ushawishi wa kumuandaa Ozil kuwa “legendari” mpya wa Emirates.

Akinukuliwa, Wenger alisema yuko katika hatua ya mwisho ya mazungumzo na straika huyo ili aweze kusaini kandarasi mpya yenye miaka kati ya mitano ama saba.

Alisema, hatua hiyo inatokana na kuamini kuwa, Ozil kwa sasa ametokea kuwa na mchango mkubwa kwa ushindi wa timu na tayari ameaminiwa na kupendwa na mashabiki wa klabu hiyo.

Aliongeza kuwa hali hiyo itamfanya aingie katika orodha ya wachezaji “malegendari” wa wakati wote hata kama atatokea kustaafu ama kuondoka emirates baadae.

“Ninaamini kuwa mazungumzo yanakwenda vizuri juu ya Ozil kuongeza mkataba mrefu. Ninamwangalia kama ndiye legendari mpya ajae ndani ya Emirates,” alisema Wenger.


Ozil mwenye umri wa miaka 28, amekuwa akisuasua katika suala la kurefusha mkataba na klabu yake hiyo huku akinukuliwa akisema, kwanza anataka kuona mwelekeo wa timu hiyo katika Ligi ya msimu huu.  

No comments