WENYE YANGA YAO WAANDAA "RUFAA" KUHUSU UAMUZI WA MANJI KUJIUZULU UENYEKITI

HATMA ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji sasa itawasilishwa rasmi katika mkutano mkuu wa klabu hiyo baada ya kamati ya Utendaji kugomea maamuzi yake ya kutaka kujiuzulu.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga inasema kuwa kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokutana jana kimebariki wanachama wa klabu hiyo wakutanishwe katika mkutano mkuu wa dharura kujulishwa juu ya Manji kutaka kujiuzulu ili nao wafanye maamuzi.

Bosi mmoja wa Yanga amesema kabla ya mkutano huo tayari kikao kilichopita cha kamati ya utendaji kiligomea maamuzi hayo na kumtaka Manji abadili maamuzi yake na kuleta mambo anayoyaona hayako sawa yaweze kujadiliwa na wanachama wa Yanga.

Alisema, mbali na kugomea maamuzi hayo, pia manji ataitwa katika mkutano huo kuweza kujibu hoja za wanachama ambao watataka kujua kiini cha maamuzi yake ili yaweze kufanyiwa kazi.

“Unajua awali tulikutana katika kamati ya utendaji mara baada ya taarifa za Manji za kutaka kujiuzulu, lakini tukakubaliana kwa pamoja kwamba hatukubaliani na maamuzi hayo na tulishamuandikia barua kabisa juu ya hilo,” alisema bosi huyo.    


“Tunataka sasa tuitishe mkutano mkuu wa dharura ili wanachama nao waambiwe juu ya hilo ili nao wafanye maamuzi ya kipirato juu ya hatma ya mwenyekiti wao lakini pia tunataka tumuite na yeye mwenyewe ili awaambie wanachama waliomchagua iweje afikie maamuzi hayo.”

No comments