YANGA KUJIPANGA KIMYAKIMYA USAJILI WA WACHEZAJI MSIMU UJAO

KATIKA kipindi hiki cha dirisha kubwa la usajili, uongozi wa klabu ya Yanga umepanga kuendesha zoezi lake kimyakimya katika kukamilisha orodha ya majina yaliyopendekezwa na kocha mkuu George Lwandamina.
Akiongea na saluti5, Katimu mkuu wa klabu hiyo, Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa mashabiki watarajie makubwa kutoka kwa Yanga kwasababu bado kuna orodha ya majina ya wachezaji wakubwa inaendelea kuwindwa.
“Niwaeleze tu mashabiki kwamba wanapaswa kutulia kipindi hiki kwani tunaendesha zoezi la usajili kimyakimya tukielekeza kila kilichopendekezwa kwenye orodha ya mwalimu,” alisema Mkwasa.
“Hatufanyi usajili kwa sifa bali ufundi zaidi ndio unaotumika, tutaweka wazi kila kitu baada ya muda mfupi kuelekea kambini,” aliongeza.

“Najua mashabiki wana shauku kubwa ya kutaka kufahamu kila hatua inayopigwa na klabu na hasa masuala ya usajili, lakini inawapasa kutambua tuko pamoja nao na tunafanya kila liwezekanalo kutimiza matakwa ya kocha,” alimaliza.

No comments