YANGA SASA WAPANIA KUMCHOMOA IBRAHIM AJIB SIMBA

BAADA ya kumkosa Mbaraka Yusuph aliyetoroshwa na Simba kupelekwa kusainishwa Azam, sasa Yanga wanataka kufanya kweli kumchomoa Ibrahim Ajib wa Simba.

Taarifa kutoka ndani ya yanga ni kwamba fungu la fedha lililokuwa limsajili Mbaraka tayari limeshaweka sawa kumsajili Ajib ambaye Simba imepotezea baada ya kutaka kiasi kikubwa cha fedha.

Bosi mmoja wa Yanga anasema Yanga ilikuwa tayari kutumia kiasi cha sh. mil 50 zilizochangwa na vigogo wa timu hiyo kwa kumsajili Mbaraka ambapo sasa wanataka kuhakikisha ndani ya wiki hii Ajib anatua Yanga.

Ajib kupitia Yanga amethibitisha kuwa Yanga imekaribia kumnasa lakini pia inajulikana kwamba Simba imemwomba mfadhili wao, Mohammed Dewji “MO” kuokoa jahazi kumalizana na Ajib pamoja na kiungo wao Jonas Mkude.

“Tunataka kufanya kweli sasa, kuna wadau wa Yanga wenye fedha zao ambao wameamua kufanya kweli kwa Ajib. Ujanua watu wamechukia Simba ilichokifanya kwa Yanga katika usajili huu wa Mbaraka sasa wamemtengea mil 50 mezani.


“Simba tunajua kwamba bado wanamtaka Ajib lakini kiasi cha fedha alichotaka ndio kikwzo kwao na wamemuomba Mo aokoe jahazi, sasa kabla ya Mo tunataka kumaliza mambo haraka.”

No comments