Habari

YANGA – TUMEPAMBANA KIUME KUMNASA KIPA YOUTHE LOSTAND

on

YANGA imepambana kiume
kujihakikishia kumnasa kipa Youthe Lostand aliyetakiwa na kocha wao, George
Lwandamina, baada ya kuingia makubaliano maalum ya kusaini mkataba wa miaka
miwili.
Taarifa kutoka ndani ya Yanga
ni kwamba jana mchana Lostand alikamilisha makubaliano ya kuingia mkataba na
Yanga baada ya majadiliano yaliyochukua wiki mbili.
Bosi mmoja wa Yanga alisema,
makubaliano hayo ya Lostand na Yanga yalifanyika chini ya usimamizi wa Katibu
mkuu wa timu hiyo, Charles Boniface Mkwasa.
Kigogo huyo alisema Lostand,
raia wa Cameroon hatua ya kukamilisha makubaliano hayo ni uhakika kwamba Yanga
imezipiga bao klabu za Azam na Simba ambazo awali zilikuwa zikimvizia kipa huyo
mgumu kufungika.
“Tulikuwa na majadiliano nae
Lostand lakini leo (juzi), tukaingia nae makubaliano ya awali kwa kusaini
mkataba wa awali ili tuwe na uhakika wa dili hili,” alisema bosi huyo.

“Unajua Lostand tulitakiwa
kupambana nae kwa udi na uvumba kutokana na kwamba yalikuwa ni mapendekezo ya
benchi la ufundi ili aje kupambania namba na makipa waliopo, Deogratias Munishi
“Dida” na Benno Kakolanya.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *