Habari

YANGA YAFANIKIWA KUMTULIZA HAJI MWINYI KIKOSINI

on

YANGA imeanza kufanya mambo kwa
utulivu ambapo Jumamosi imefanikiwa kumbakisha beki wake wa kushoto Haji Mwinyi
kisha ikamalizana na kiungo aliyetakiwa na kocha wao George Lwandamina na
kuachana na Salmin Hoza.
Aliyefanya kazi hiyo ya
kumsainisha Mwinyi aliyekuwa akiviziwa na Azam na mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili Hussein Nyika akisaidiana na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface
Mkwasa ambapo beki huyo amesaini mkataba mpya wa miaka miwili.
Mwinyi aliyesafirishwa jana
kutoka kwao Zanzibar na kufika jana mchana ambapo haraka jana hiyohiyo
akakubali kubaki Yanga ambapo sasa anatafutiwa beki mwingine atakayechuana nae.
Wakati Yanga ikianza hivyo,
tayari klabu hiyo imefanikiwa kumsajili kiungo wa Mbao, Pius Buswita na
kufanikiwa kuwapigisha chenga Azam waliomnyakuwa Salmin Hoza ambaye alikuwa
akitakiwa kusajiliwa Yanga kwa ziada tu.
Katika ripoti ya kocha Lwandamina
kiungo muhimu aliyekuwa akimtaka kutoka Mbao ni Buswita lakini Yanga
ikawapigisha chenga Simba na Azam kwa kutangulia kufanya mazungumzo na Hoza
ambaye walimkimbilia kisha kumwacha Buswita ambaye sasa ni mali ya Yanga.
“Tumemalizana na Mwinyi,
tulimwita haraka na Jumamosi tukamalizana nae, amesaini mkataba mnono wa miaka
miwili kwa hiyo hatuna mashaka nae tena,” alisema bosi huyo.

Ukiacha Mwinyi pia tumemsajili
kiungo fundi wa Mbao, Pius Buswita ambae ndie kiungo mwafaka tuliyekuwa
tukimtaka lakini tulijua kwamba hizi timu nyingine zinasubiri kusikia nini
Yanga wanataka kufanya ili wao wakimbilie sasa tulipomtaja Hoza wao
wakakimbilia kumsajili lakini tukafanikiwa kumpata Buswite tuliekuwa na mipango
nae.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *