YANGA "YAUKATAA" MKATABA WA SPORTPESA ULIOMWAGIKA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

MAKAMU mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga amekanusha habari zilizoenea kwenye mitandao kuhusiana na mkataba wa ufadhili wa Sportpesa ambao umeenezwa kwenye mitandao ya kijamii nchini.

Sanga amesema kuwa mkataba huo ni feki ukiwa na lengo la kuchafua hadhi ya klabu hiyo iliyobeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa tatu mfululizo.

“Tumeingia mkataba kihalali kabisa na kampuni ya Sportpesa na kila kitu kiko wazi kwenye ofisi ya Katibu mkuu, Charles Mkwasa. Huo mkataba uliowekwa kwenye mitandao hatuhusiani nao,” alisema Sanga.

“Ni mkataba wenye manufaa pande zote mbili, kama kuna mwanachama ana mashaka na mkataba huo aende kwenye ofisi ya Katibu Mkuu apewe nakala ausome,” aliongeza.

“Yanga ni bland kubwa haiwezi kuingia kwenye mikataba kiholela ya kutokuwa na faida na klabu, tuna uzoefu wa vitu vya namna hii. Klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya Sportpesa.”


“Tunaomba utulivu kwa wanachama kwa sababu klabu ipo kwenye kipindi cha usajili wa wachezaji wapya kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi na michuano ya kimataifa,” alimaliza Sanga.

No comments