YANGA YAVUTA WAGENI WAWILI KUZIBA PENMGO LA HARUNA NIYONZIMA

YANGA imevunja benki kusajili viungo wawili wa kigeni ambao wanakuja kuziba pengo la Haruna Niyonzima ambaye huenda akahamia Simba kwa msimu ujao.

Taarifa kutoka kamati ya usajili ni kwamba tayari kocha mkuu wa Yanga, George Lwandamina ameshajulishwa juu ya Niyonzima kuondoka klabuni ambapo ametuma jina la kiungo fundi wa kikosi cha timu ya taifa ya Zambia kuja kuchukua nafasi hiyo.

Lwandamina amekabidhi jina hilo kwa katibu mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa ambapo tayari kazi imeshaanza kuhakikisha anakuja kuchukua nafasi hiyo ya Niyonzima.

Wakati kiungo huyo mchezaji akianzishiwa mazungumzo hayo, huku nyuma mshambuliaji wa Yanga, Amisi Tambwe nae amependekeza jina la kiungo mmoja mkabaji ambaye ameonyesha ni shoka katika ukabaji.

Tambwe ametuma jina hilo haraka kwa mabosi wa Yanga akiwataka kutofanya makosa katika kumnasa kiungo huyo ambaye pia yumo katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo.


Tayari wawili hao wanaonyesha ushirikiano mkubwa wa kuweza kutua kutokana na kutotaka gharama kubwa katika kutua Jangwani.

No comments