ZANZIBAR STARS MPYA SASA NI DDC KARIAKOO KILA JUMANNE

ZANZIBAR Stars Modern Taarab iliyorejea upya na kwa kishindo hivi sasa, kuanzia wiki ijayo itakuwa ikipatikana ndani ya DDC Kariakoo, katika siku za Jumanne, imefahamika.

Akiongea na saluti5, bosi wa Zanzibar Stars Modern, Juma Mbizo amesema kuwa hatua ya bendi hiyo kupanga kutumbuiza DDC Kariakoo imekuja kufuatia maombi mengi ya mashabiki wao.

Mbizo amesema kuwa, mashabiki wao wa katikati ya jiji wamependekeza kuwepo kwa shoo japo moja ya kudumu itakayokuwa inawakutanisha kwa pamoja wadau na wamepnzi wa bendi hiyo hata mara moja tu kwa wiki.

“Tumepanga kuwafikia mashabiki wengi wa maeneo tofauti kwa kutumbuiza kwenye kumbi mbalimbali za jijini Dar es Salaam hata nje ya mji, lakini kwa sasa tunaanza na shoo hiyo itakayokuwa kali zaidi,” amesema Mbizo.


“Kiingilio katika shoo hiyo itakayokuwa ikianza kuunguruma majira ya saa 3:00 usiku na kuendelea hadi majogoo, kitakuwa ni sh. 5,000 tu kwa mtu mmoja,” amesema Mbizo na kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi.

No comments