4 STARS BAND YA NASSOR DIMOSO KUIVURUGA BEST POINT HOTEL UBUNGO IJUMAA HII

4 Stars Band iko katika viwanja vya Best Point Hotel, Ubungo, Dar es Salaam Ijumaa hii ambapo itaungurumisha burudani kali ya muziki mchanganyiko kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Bosi wa 4 Stars, Nassor Dimoso aliieleza Saluti5 kuwa hiyo ni fursa pekee kwa mashabiki wao wa Ubungo na maeneo jirani kufaidi ladha ya mambo yao matamu waliyowaandalia ambayo ni muziki wa kiutu uzima zaidi.

“Shoo itaanza majira ya saa 1:00 jioni na kuendelea hadi majogoo huku kiingilio kikiwa bure, tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuianza wikiendi kwa kuburudisha zao na muziki huu ambao si wa kawaida,” amesema Dimoso.


4 Stars ni kati ya bendi tishio zinazotumbuiza muziki wa kimataifa kutoka katika nchi mbalimbali duniani, ambayo inakusanya wanamuziki wenye uwezo mkubwa na waliowahi kutamba kwenye bendi maarufu Bongo.

No comments