AC MILAN YAKAMILISHA KUINASA SAINI YA STRAIKA WA ZAMANI WA LIVERPOOL

KLABU ya AC Milan imeendelea kufanya fujo zao za usajili na wamekamilisha dili lingine la kuinasa saini ya straika wa zamani wa Liveerpool, Fabio Borini.

Mtandao wa Goal.com uliripoti kuwa straika huyo alitarajiwa kufanyiwa vipimo kabla ya kutinga uzi wa Milan akitokea Sunderland alikocheza mechi 24 na kufunga mabao mawili tu kabla ya kushuhudia timu hiyo ikishuka daraja msimu uliopita.


Kabla ya kuzishezea Liverpool na Sunderland, Borini alianza soka lake akiwa Chelsea kabla ya kutimkia katika klabu za Parma na kisha Roma, zote za Ligi Kuu Italia “serie A”  

No comments