ALEX SANDRO ATAKA KUSEPA JUVENTUS ILI ATUE MANCHESTER CITY

ALEX Sandro tayari ameonyesha azma ya kutaka kuondoka Juventus ili akatafute maisha mbele ya safari katika usajili huu wa majira ya kiangazi.

Tena amekwenda mbali zaidi kwa kuitaja timu anayoipenda kwenda kukipiga na kwamba mapenzi yake ni kuvaa uzi wa Manchester City.

Mshambuliaji huyo ameuomba uongozi wa klabu ya Juve licha ya kumruhusu aondoke, anataka kwenda kutimiza azma yake ya kucheza Ligi ya premier.

Sandro ambaye msimu huu amekuwa katika kiwango bora akiwa Juve, ameweka bayana ndoto yake ya kucheza katika Ligi iliyo na mashabiki wengi.

“Nina malengo ya kutimiza ndoto   ya kwenda kucheza katika Ligi ya premier.”

“Ninataka kuona ninalinda kipaji changu, sitaki kuwa msiri juu ya hili la mimi kuondoka hapa.”

“Soka ni kazi ninayoenda kuifanya kokote. Ni mchezo wa kuangalia leo na kesho. Huu ndio msimamo wangu kwa sasa,” alisema Sandro.

“Manchester City ni klabu ninayoipenda kwa ajili ya soka langu la baadae. Ninaamini nina nafasi ya kucheza nikiwa kule na kutimiza ndoto yangu hii,” alisisitiza Sandro raia wa Brazil.


No comments