ALEXIS SANCHEZ AIPASUA KICHWA ARSENAL


ARSENAL ina wasiwasi kuwa straika wake Alexis Sanchez yu tayari kuondoka kwa uhamisho huru kiangazi kijacho.

Sanchez anaingia katika miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake Emirates, huku kukibaki maswali juu ya mustakabali wake.

Staa huyo wa kimataifa wa Chile amekiri kuwa tayari amefanya uamuzi kuhusu mustakabali wake na wiki ijayo atatangaza alichoamua.


Lakini gazeti la The Sun limesema kuwa Arsenal ambayo ina nia ya kumbakisha staa huyo Emirates, bado imebaki kizani kuhusu nini anataka kukifanya.

No comments