ALVARO MORATA MBIONI KUTUA AC MILAN KWA PAUNI MIL 61


AC Milan inakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata kwa pauni milioni 61.

Gazeti La Gazzetta dello Sport la Italia limedai Real Madrid imekubali kupunguza dau walilotaka la pauni milioni 79 kwa mshambuliaji huyo aliyekuwa lengo kuu la usajili la Manchester United kiangazi hiki, kabla haijageuza nguvu zao kwa Romelu Lukaku.

Chelsea nayo ilikuwa ikimpigia hesabu Morata baada ya kuzidiwa ujanja na Manchester United kwenye usajili wa Lukaku.
No comments