AMISSI TAMBWE AJIFUA KIVYAKE KUJIANDAA NA CHANGAMOTO YA LIGI KUU

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe raia wa Burudni amesema kuwa anafahamu ugumu wa ratiba waliyopangiwa na upinzani watakaokabiliana nao kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu bara, hivyo amekuwa akitenga muda wa ziada kujiweka fiti.

Tambwe amesema kwamba msimu ujao unaweza kuwa na tofauti kubwa ukilinganisha na msimu uliopita kwa sababu timu nyingi zinafanya vizuri sokoni na hata wachezaji wenyewe hawajapoa, kila siku wapo uwanjani.


“Ni rahisi tu kutabiri kwamba msimu ujao utakuwa mgumu kwa sababu ya usajili unaofanywa na baadhi ya timu zilizopanda daraja na hata zile zilizopo, lakini pia wachezaji hawajapumzika tangu msimu umalizike, kila siku wapo uwanjani kwenye majukumu na timu zao za taifa,” alisema Tambwe. 

No comments