ANCELOTTI AUSHANGAA UWEZO WA MANUEL NEUER NA KUSEMA SI BINADAMU WA KAWAIDA

KOCHA wa Bayern Munich, Carlo Ancelotti  amedai kuwa mlinda mlango wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Ujerumani, Manuel Neuer anaweza kuwa sio binadamu wa kawaida ila atakuwa na kompyuta kichwani kwake.

Ancelotti amesema uwezo wa kipa huyo ni mkubwa sana na mchango wake umeifanya klabu hiyo kutwaa mataji sita mfululizo ya Ligi Kuu nchini Ujerumani.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ujerumann ambaye amefunga ndoa siku za hivi karibuni bado ni majeruhi kutokana na kusumbuliwa na goti lakini kuna uwezo kano mkubwa wa kuwa fiti katika mchezo wa kwanza wa ufungaji wa Ligio Kuu nchini humo dhidi ya Bayern Leverkusen.

“Kwenye kikosi chetu tunayo kompyuta gorini ambaye ni mlinda mlango Neuer huyu ni kipa wa pekee kwenye ulimwengu wa sasa yupo tofauti na makipa wengine ambao nimekutana nao kwa miaka ya hivi karibuni.

“kuna wakati naweza kusema mchezo huo hana mikono kifua na miguu lakini anayo ‘Keyboard’ ya komputera kwenye kichwa chake katika kila mchezo akiingia uwanjani.

“Sina wasiwasi na uwezo wake kwa kuwa mchango wake ndani ya klabu na timu na timu ya taifa ya ujerumani umekuwa mkubwa sana basdo ana nafasi kubwa ya kuweka histori ya aina yake kwenye soka alisema Ancelotti.

No comments