ANTONIO CONTE MASHAKANI CHELSEA

INAWEZA kuwa habari mbaya sana kwa mashabiki wa klabu ya Chelsea, lakini pia inaweza kuwa habari ambayo haiwezi kuwashitua baadhi yao.

Tangu alipomuandikia meseji ya simu mshambuliaji wake, Diego Costa kwamba hamtaki tena kwenye klabu hiyo, kocha wa timu hiyo Atonio Conte amekuwa kama amechokoza nyuki mzingani.

Mashabiki wengi wa Chelsea wamekuwa wakilalamika kwamba kwanini kocha huyo anamuondoa mtu ambaye amekuwa akikutana na nyavu kila wakati, lakini sasa mambo yanaonekana kama yamemgusa moja kwa moja kocha huyo.

Juzi kutwa nzima kumekuwa na habari kwamba sasa ni dhahiri mustakabari wa Antonio Conte uko mashakani baada ya meneja huyo kukasirishwa na shughuli nzima ya usajili katika klabu hiyo.

Gazeti la Daily Mirror limeandika kwamba kocha huyo anapinga kuingiliwa katika mambo ya usajili kukiwa na habari kwamba wenye timu wanaona kwamba wasipotia miguu kwenye usajili Conte anaweza kuwaharibia.

Sasa imedaiwa kuwa huenda kocha huyo akavunja mkataba ikidaiwa anaona kwamba anafanya kazi chini ya usimamizi mkubwa ambao unamnyima amani.


Pamoja na kwamba habari hii inafanywa kuwa siri, lakini kocha huyo amekuwa akidaiwa kuwa ameshawaambia marafiki zake kwamba maisha yake katika klabu hiyo huenda yakawa mafupi sana.

No comments