Habari

ARSENAL KUMBAKISHA WILSHERE UINGEREZA KWA MAJERAHA YA MGUU

on

KLABU ya Arsenal inajipanga
kumwacha kiungo wao Jack Wilshere nchini England ambako ataendelea kuuguza
maumivu yake ya mguu uliovunjika, hali itakayomkosesha nafasi ya kuichezea timu
yake kwenye pre-season Australia na China.
Kiungo huyo alipata jeraha hilo
msimu uliopita na kujikuta akikosa wiki za mwisho za kuibeba timu aliyokuwa
akiiochezea kwa mkopo ya Bournemouth.
Wilshere atafanyiwa scan siku
chache zijazo ili kuchunguza maendeleo ya jeraha lake kabla ya kuruhusiwa
kuanza mazoezi ya taratibu.

Kama kila kitu kitaenda vizuri,
kiungo huyo ataanza mazoezi na klabu yake pindi atakaporudi London.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *