ARSENAL KUPIMANA UBAVU NA MAN CITY KWA VIRGIL VAN DIJK


ARSENAL imeripotiwa kujiunga katika mbio za Chelsea, Liverpool na Manchester City kumuwania beki wa Southampton raia wa Uholanzi, Virgil van Dijk.

The Gunners inaweza kujikuta ikivunja rekodi yake ya uhamisho kwa mara ya pili kiangazi hiki ili kufanikiwa kumpeleka beki huyo wa kati Emirates Stadium, kutokana na taarifa ambazo hazijathibitishwa, kueleza kuwa anaweza kugharimu kati ya pauni milioni 60 na 70.

Rekodi ya Arsenal wakati ikiingia katika usajili kiangazi hiki ilikuwa pauni milioni 42 ilizotoa kumsajili Mesut Ozil mwaka 2013, lakini ikavunjwa na ujio wa Alexandre Lacazette kutoka Lyon aliyegharimu karibu pauni milioni 50.

Arsenal inataka kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa kuwa Shkodran Mustafi hakuwa na la maana baada ya kusajiliwa kutoka Valencia kiangazi kilichopita, Laurent Koscielny na Per Mertesacker wamekuwa wakihangaika na majeruhi na kinda Rob Holding akikosa uzoefu licha ya kufanya vizuri kuelekea mwisho wa msimu uliopita.

No comments