ARSENAL WAONGEZA OFA KWA AJILI YA KYLIAN MBAPPE

KWA lugha nyingine unaweza kusema ni kama wameamua baada ya kuwepo na ripoti zinazodai kwa Arsenal wameamua kuongeza ofa yao kwa ajili ya kumnasa straika wa AS Monaco Kylian Mbappe.

Kwa mujibu wa habari mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 ndiyo shabaha ya kwanza kwa bosi wa Arsenal Arsene Wenger na Real Madrid lakini bado mustakabali wake haujaeleweka kwani Monaco wanafanya jitihada za kumbakisha kwa ajili ya msimu ujao.

Hata hivyo kwa mujibu wa Marca, miamba hao wa Ligi Kuu Uingereza wameongeza ofa yao hadi pauni mil 123 kiwango ambacho kitaizidi rekodi kubwa kwa sasa inayoshikiliwa na Manchester United kwa kumsajili Paul Pogba kutoka Juventus.

Haijawahi dhahiri kwamba Mbappe angependelea kutua Emirates au Bernabeu lakini Arsenal wanaweza kumpa majukumu makubwa kuliko Real Madrid yenye wachezaji wakali kama Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na Karim Benzema ambao hawana dalili za kuondoka Hispania.

Msimu uliopita Mbappe alifunga mabao  15 katika mechi 29 Monaco wakishinda League 1 na alifunga mabao 6 zaidi katika mechi 9 klabu yake ikifika nusu fainali ya Ulaya.


Klabu nyingine zenye nia ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa lakini Arsenal na Real Madrid ndizo zenye nafasi kubwa kumpata.

No comments